Usain Bolt ashinda dhahabu yake ya tatu Rio
Shindano la Bolt la mwisho lilikuwa la mita 100 kupokezana vijiti mara nne
Mwanariadha
wa kasi zaidi duniani mzaliwa na Jamaica Usain Bolt amepata dhahabu
katika mbio tatu tofauti katike kile kinachojulikana katika kiingereza
kama "trible trible" au tatu tatu.
Shindano lake la mwisho lilikuwa la mita 100 kupokezana vijiti mara nne.
Alipokea
kijiti mwisho katika timu yake na akafululiza kishujaa na kumshinda
mpinzani wake wa karibu kutoka Japan, aliyeshinda Marekani na kuchukua
Shaba.
Bolt
ameshinda dhahabu mara tatu katika Olimpiki zote tatu alizoshiriki ndipo
ushindi wake huu ukatambuliwa kama trible trible yaani tatu tatu.
Ushindi wa Usain Bolt unakuja siku tatu kabla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa
Bolt
mwenye umri wa miaka 29, alishinda dhahabu katika mbio za mita 100 na
200 mjini Rio na ndiye mwanariadha wa kwanza kushinda mbio tatu katika
mashindano matatu ya olimpiki
Awali timu ya marekani ya wanawake ilishinda mbio sawa na hizo za kupokezana vijiti.
No comments: