FEDHA ZA MAENDELEO KUUNGUZA WATAKAOZICHEZEA - WAZIRI MKUU
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji wa halmashauri mkoani Katavi
kuwa makini na matumizi ya fedha za maendeleo zinazopelekwa katika
maeneo yao na atakayethubutu kuzichezea zitamuunguza.
“Fedha
hii tafadhali ni ya moto. Msicheze na hii ya halmashauri tunayoileta
hapa halmashauri kwa ajili ya wananchi itawakunguza vidole. Tunaileta
kwa madhumini, tunataka wananchi wahudumiwe,“ alisema.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Agosti 21, 2016) wakati
akihutubia umati mkubwa wa wananchi kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kiwanja cha Azimio wilayani Mpanda.
Alisema
Serikali imeanza kupeleka fedha za miradi ya maendeleo katika
halmashauri mbalimbali hivyo ni vema kila mtendaji ahakikishe fedha hizo
zinatumika kwa ajili ya ujenzi wa miradi iliyokusudiwa na si
vinginevyo.
Waziri
Mkuu alisema ni lazima wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri
wahakikisha viwango vya ubora wa miradi inayojengwa katika maeneo yao
kuwa inalingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwenda wilayani Mpanda na
kuangalia namna ya kuipanua hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambayo
inahudumia mkoa wote wa Katavi.
Alisema
hospitali hiyo ilijengwa mwaka 1957 kama zahanati ambayo kwa sasa
yanatumika katika kuwahudumia wananchi wate wa mkoa huo imezidiwa hivyo
alimuagiza mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga
kuharakisha ujenzi wa hospitali ya mkoa.
Aidha,
Waziri Mkuu alisema kuwa wakati mkoa ukiwa kwenye harakati za ujenzi wa
hospitali ya mkoa wilaya nazo zianze ujenzi wa hospitali za wilaya ili
kuhakikisha sera ya Serikali ya kuwa na hospitali katika kila wilaya
inatekelezwa.
Alisema
kwa sasa madaktari na wauguzi wanaofanya kazi kwenye hospitali ya
Manispaa ya Mpanda wamezidiwa kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya
wagonjwa kuliko uwezo wao. Hivyo amewataka madaktari na wauguzi wa
wilaya ya Mpanda kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wenzao wa
Manispaa.
Awali
hospitali hiyo ilikuwa chini ya uongozi wa halmashauri ya Mpanda.
Hospitali hiyo kwa sasa ipo chini ya Manispaa ya Mpanda hivyo Waziri
Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa huo kuboresha huduma kwa kupeleka dawa na
vifaa tiba vitakavyoweza hospitali hiyo kuhudumia wagonjwa wa mkoa.
Mkoa umetenga sh. bilioni 1.7 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya mkoa.
Wasanii
wa kijiji cha Katumba wilayani Mpanda wakicheza ngoma ya Kasimbo
wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara
kijijini hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia kwake) wakiwapungia
wananchi wa Mpanda wakati walipowasili kwenye uwanja wa Kashaulili
mjini Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti21, 2016.
Wananchi
wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili
kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara
Agosti 21, 2016. Katika hotuba yake Waziri Mkuu alizitolea majibu kero
zote zilizoandikwa kwenye mabango hayo akiwahusisha watendaji wa
Halmashauri, mkoa na wilaya.
Mke wa
Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mpanda wakati
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye
uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda Agosti 21, 2016. Kulia ni Mkuu wa mkoa
wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Mbuga.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda Agosti 21, 2016.
No comments: