Header Ads

Seo Services

Bora kubaki unapopajua kuliko kuhamia usipopajua

healthycouple-lifemagKWA neema na rehema zake Mwenyezi Mungu tunakutana tena katika safu hii ya Love and Story. Kwa wale tunaopenda kujifunza kila siku kitu kipya, hili ni eneo zuri sana la kuweza kujifunza na kuweza kupata jambo jipya linaloweza kutusaidia katika maisha yetu ya uhusiano.

Kwa tuliokuwa pamoja wiki iliyopita tulijifunza juu ya umuhimu wa kupeana nafasi na mpenzi wako pale mnapoona mambo hayaendi sawa. Mnaachana kwa muda kisha mnarudiana. Nilisema kufanya hivyo kunasaidia wapendanao kujitathmini kubaini udhaifu na mnaporudiana penzi linakuwa motomoto kwani kila mmoja wenu anakuwa ameshajifunza.

Tukirudi katika somo la leo, ni vyema tukatambua umuhimu wa kuthamini pale ulipo. Kubaki na mpenzi unayemjua kuliko kutafuta mpya. Wapya wana madhara yake. Twende pamoja…
Katika kizazi cha sasa, watu wengi wamekuwa si wavumilivu. Wanataka kuishi kwenye uhusiano ambao utakwenda vizuri bila kupitia mgogoro wowote. Yaani akikutana na tatizo dogo tu, anaamua kuachana na mwenza wake na kuhamia kwa mtu mwingine.

Kwa wanawake wa mjini huwa wana misemo yao kama vile; “Babu eeh kwani wanaume wameisha duniani? Nenda mwana, nitapata mwingine. Mwanaume haupo peke yako.
wanza mtoto wa watu sina kasoro, naita navutia, wanaume kibao wananishobokea.”

Kwa wanaume nao pia wapo wanaotoa kauli zao. Utawasikia wakisema; “Mwanaume ni mwanaume tu. Sisi ndiyo kila kitu. Nakuwa na wewe, ukizingua napiga chini nahamia kwa mwingine. Mwanamke unatakiwa umnyenyekee mwanaume sababu kwanza ndiye anayeoa. Wanawake wapo wengi, nafanya kuchagua yupi niwe naye, yupi nimchezee na yupi nimuoe.”

Kauli kama hizo na nyingine nyingi huwa zinatokana na kiburi cha uzima. Kwamba kila mmoja anaringia kile alichonacho kumuadhibu mwenzake, akiamini kwamba ana mkomoa. Kwa vile kweli anavyojivunia navyo vipo chini ya uwezo wake.

Kwa sababu kweli ana mvuto, mwanamke anaweza kupata kweli mwanaume mwingine. Tena ndani ya muda mfupi tu baada ya kuachana na mwanaume wa awali. Na hata yule mwanaume kwa sababu ana mvuto, ana fedha pengine, anaweza kumpata mwanamke ndani ya muda mfupi tu.
10-couple-by-the-beach-mainMarafiki zangu, mapenzi yana maana pana. Mapenzi si tu kumalizana matakwa ya matamanio ya kimwili. Mapenzi ni utu. Mapenzi ni kuelewana. Kusaidiana katika shida na raha. Kupendana. Kuheshimiana. Kusomana kitabia na maisha kwa ujumla.

Ni dhahiri kwamba unapokuwa na mwenzako kwa kipindi fulani, unamzoea. Unajua ana tabia gani. Kipi hakipendi na kipi anakipenda. Unajua kwamba ili muishi kwa amani, hupaswi kumfanyia kitu gani. Mnakuwa mnapendana maana mmeshatengeneza historia fulani, hata kama ni ndogo.

Historia mnayokuwa mmeitengeneza ni muunganiko wa kuendana (chemistry). Si rahisi sana kuipata sehemu nyingine. Hapo ndipo kwenye kiini cha mada yangu. Heshimu hiyo chemistry uliyoitengeneza. Ni rahisi kuiboresha kuliko kwenda kuanzisha mpya.

Itakuchukua muda tena kuitengeneza. Mbaya zaidi hautakuwa na uhakika nayo.
anasana unaweza kujikuta ukiambulia maumivu. Utaingia kwenye uhusiano usiokuwa na kichwa wala miguu. Utapoteza uelekeo.Utakuwa mtu wa kutangatanga bila sababu ya msingi. Ni bora kurekebisha pale ulipo. Pang’ang’anie hadi uone mwisho wake. Siyo umeudhiwa kidogo, unaona njia pekee ya kuwa salama ni kuachana na mpenzi uliyenaye.

Unafikiri unakokwenda ndiyo salama? Nani kakuhakikishia? Tetea kwa nguvu zote uhusiano ulionao kama unaamini ni sahihi. Usikubali kuyumbishwa. Huyo mliyesomana tabia ana umuhimu kwako kuliko yule unayekwenda kujifunza kumsoma tabia.

No comments:

Powered by Blogger.