MATANGAZO John Kerry aitaka Sudan Kusini kukubali wanajeshi 4000 wa UN
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry
Waziri wa
maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry ameitaka Sudan Kusini
kuwakubali wanajeshi 4000 wa Umoja wa Mataifa nchini humo.
Akizungumza
baada ya kukutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mawaziri wa
maswala ya kigeni jijini Nairobi,Kerry amesema kuwa Sudan Kusini inafaa
kuheshimu makubaliano ya amani nchini humo kwa maneno na vitendo ili
kuhakikisha kuwa yanaafikiwa.
Amewataka viongozi wa taifa hilo kutojihusisha na vitendo vya ghasia ambavyo vinaweza kuchangia vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mapema mwezi huu Sudan Kusini ilisema kuwa haitashirikiana na Umoja wa Mataifa .
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Bwana
Kerry pia amesema kuwa mafanikio makubwa yameafikiwa katika kukabiliiana
na tishio la wapiganaji wa kundi la al-Shabab nchini Somalia,lakini
mengi yanahitajika kufanywa katika eneo hili.
Ameongezea kuwa Marekani itaahidi dola milioni 138 za misaada ya kibinaadamu kwa Sudan Kusini mwaka huu.BBC
No comments: