TUTAWANYANG’ANYA URAIA TULIOTOA KWA WAKIMBIZI WATAKAOBAINIKA KUTUUMIA VIBAYA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mnara uliojengwa na
wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania ili kumshukuru Mungu kwa kupewa
urais huo wakati alipokitembelea kijiji Katumba mkoani Katavi Agosti
21, 2016. Kushoto kwake ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Mbuga. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakifurahia baada ya kuzindua mnara
uliojengwa
na wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania ili kumshukuru Mungu kwa
kupewa urais huo wakati Waziri Mkuu alipokitembelea kijiji Katumba
mkoani Katavi Agosti 21, 2016. Kushoto kwake ni mkewe Mary na kushoto i
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Mbuga. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzindua mnara
uliojengwa na wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania katika kijiji cha
Katumba mkoani Katavi Agosti 21, 2016 ili kumshukuru Mungu kwa kupewa
uraia huo. Kushoto kwake ni mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa mkoa wa
Katavi, Meja Jenerali Raphael Mbuga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Makazi ya Wakimbizi ya
Katumba mkoani Katavi, Bwbana Igwe baada ya kuwasili kambini hapo
kuzunguma na wananchi akiwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21,
2016. Wapili kulia ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa kijiji cha Katumba mkoani
Katavi wakati alipoingia kwenye kijiji hicho kuzungumza na wananchi
akiwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016. Kulia kwake ni
Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Raphael Mbuga. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Mpango wa Mafunzo ya Ujasiriamali
katika jimbo la Nsimbo mkoani Katavi aliouzindua kabla ya kuhutubia
mkutano wa hadhara katika kijiji cha Katumba akiwa katika ziara ya mkoa
huo Agosti 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkuano wa hadhara katika kijiji cha
Katumba mkoani Katavi Agosti 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya
wananchi wa kijiji cha Katumba mkoani Katavi wakimsikiliza Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo
akiwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya
baiskeli za wananchi wa kijiji cha Katumba wilayani Mpanda
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano
wa hadhara kijijini hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania
na kuitumia vibaya nafasi hiyo kwa kuingiza watu wengine kinyume cha
sheria watanyang’anywa na kurudishwa walikotoka.
Aidha,
Waziri Mkuu amewaomba viongozi wa dini wawe wanawaelimisha waumuni wao
umuhimu wa kulinda amani na kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za
nchi husika.
Kauli
hiyo imetolewa leo (Jumapili, Agosti 20, 2016) na Waziri Mkuu wakati
akizungumza na waliokuwa wakimbizi wa Burundi ambao kwa sasa wamepewa
uraia wa Tanzania wanaoishi katika Kata ya Katumba, Halmashauri ya
Nsimbo wilayani Mpanda.
“Wakimbizi
waliopewa uraia wameendelea kuingiza ndugu zao. Naagiza kamati ya
ulinzi na usalama ya mkoa ifanye ukaguzi katika kambi zote kwa sababu
zimegeuzwa kuwa maficho ya kuwahifadhi watu wanaoingia nchini bila ya
vibali,” amesema.
“Hakikisheni
mnachukua hatua kwa wote watakaoingiza watu kinyemela katika kambi za
wakimbizi za Mishamo na Katumba. Pia msiruhusu watu kuleta silaha kwenye
maeneo haya. Tanzania watu wanaoruhusiwa kutembea na silaha ni askari
tu,” amesisitiza.
Waziri
Mkuu amesema lazima ulinzi uimarishwe katika maeneo ya mipakani na
wasipofanya hivyo watu wengi wataingia nchini bila ya kuwa na vibali
hivyo kusababisha ongezeko kubwa la idadi ya watu.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda
wasiwaudhi wakulima na wafanyabiashara wadogo kwa kuwatoza ushuru
kwenye mazao wanapotoka shambani kama debe moja la nafaka na wanaouza
bidhaa ndogo ndogo.
“Mkulima
ametoka shambani na debe moja la mahindi unamtoza ushuru maana yake
nini? Halmashauri tusitafute mgogoro katika hili. Tafuteni biashara za
kutoza ushuru, mkulima anatoka kijiji cha Kanoge anakwenda kijiji cha
Ikongo ushuru wa nini? Waziri Mkuu amehoji.
Waziri
Mkuu amesema “Tumewasisitiza mkusanye kodi lakini siyo hivyo. Mkiendelea
kutoza ushuru kwa wakulima wanaotoka shambani na mahindi kidogo
mtasababisha wakate tamaa ya kulima,”.
Akisoma
taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Katavi jana jioni (Jumamosi, Agosti 20,
2016) mara baada ya Waziri Mkuu kuwasili mkoani hapa Mkuu wa mkoa, Meja
Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga alisema mkoa una jumla ya wakimbizi
6,918 wanaoishi katika kambi za Mishamo na Katumba ambapo kati yake
wakimbizi 2,150 waliomba uraia wa Tanzania na kunyimwa.
Alisema
wakimbizi 2,489 walichagua kurejea nchini kwao Burundi ila bado wapo
katika kambi hizo huku wengine 653 waliomba uraia lakini majina yao
hayakuonekana kwenye orodha ya waliokubaliwa wala kukataliwa uraia hivyo
mkoa unaendelea kufuatilia ili kujua hatma yao.
Mkuu huyo
wa mkoa alisema kuwa wakimbizi wengine sita walichagua kubaki nchini
lakini hawakuomba uraia, 398 waliomba uraia ila fomu zao
hazikukamilika,249 waliomba uraia ila majina yao hayakurudi huku wengine
973 hawakusajiliwa walipoingia nchini mwaka 2007/.2008
No comments: