Taarifa ya Jeshi la Polisi Kwa Vyombo Vya Habari
Katika
siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa
jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi katika
maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kufuatia
hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu
wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi
Aidha,
jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za
kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali
zinazofanywa na wananchi.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.
No comments: