UTOAJI WA MALALAMIKO NA KERO JUU YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI PAMOJA NA MASUALA YA JINSIA, WAZEE NA WATOTO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na
kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha
utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali
na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.
Katika utekelezaji
huu, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana lakini pia zipo changamoto mbalimbali
zinazojitokeza katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini. Baadhi ya
changomoto hizo ni za kiutendaji zaidi ambazo zinaweza kutatuliwa kwa haraka
endapo tutaimarisha usimamizi na uwajibikaji katika kila ngazi kuanzia ngazi ya
Wizara, Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za afya. Changamoto hizi ni pamoja na wagonjwa kutopatiwa huduma haraka
na sahihi, lugha na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma na makundi yanayotakiwa
kupata matibabu bure (yaani Wazee, Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya
miaka 5) kutozwa fedha kinyume na Sera ya Afya ya 2007). Takribani kila
siku vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio kadhaa kuhusu malalamiko na
kero mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi
katika kupata huduma za afya.
Wasimamizi
wa Wakuu wa Utekelezaji wa Sera na Miongozo ya Afya katika ngazi ya Mikoa ni
Waganga Wakuu wa Mikoa. Ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya
pamoja na kuhakikisha malalamiko na kero zao zinashughuhulikiwa kwa haraka, Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) ameamua kuweka wazi namba za simu za
Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO) wote nchini ili wananchi wanapokuwa na
malalamiko/kero waweze kuwasiliana nao moja kwa moja. Mhe Waziri amewataka
Waganga Wakuu wa Mikoa kuyafanyia kazi masuala yote yanayoletwa na wananchi
katika Mikoa yao na kuyapatia ufumbuzi haraka. Hivyo, wananchi wasisite
kuwasiliana nao kupitia namba zao zifuatazo pamoja na kwa barua pepe.
Katika muktadha
mzima wa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Sheria na Sera za Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, mwananchi yoyote ambae ana
malalamiko, maoni au ushauri kuhusu sekta husika unaweza kuwasiliana moja kwa
moja na Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (Mb) kupitia simu namba 0746 – 505030 (kwa njia ya ujumbe) pamoja
na kueleza mkoa uliopo, twitter @wamjw na email: waziri@moh.go.tz
“Uwazi na Uwajibikaji ni chachu ya kuleta mabadiliko
katika sekta ya afya, sambamba na kulinda Haki za Watoto, Wazee na Wanawake”.
MAWASILIANO NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA (RMOs)
NA.
|
MKOA
|
JINA
LA MGANGA MKUU
|
NAMBA
YA SIMU
|
NUKUSHI
|
1.
|
ARUSHA
|
DKT. FRIDA MOKITI
|
0784-264750
|
fridamokiti@yahoo.com.
|
2.
|
DAR ES SALAAM
|
DKT. GRACE MAGEMBE
|
0767-300234
|
magembegrace@yahoo.com
|
3.
|
DODOMA
|
DKT. JAMES CHALRES
|
0784-504955
|
jcrexford@yahoo.com
|
4.
|
IRINGA
|
DKT. ROBERT M. SALIM
|
0754-377176
|
saludimwe@yahoo.com
|
5.
|
KAGERA
|
DKT. THOMAS RUTACHUNZIBWA
|
0754-803729
|
thomasruta@yahoo.com
|
6.
|
KIGOMA
|
DKT. PAUL CHAOTE
|
0755-696855
|
pchaote@gmail.com
|
7.
|
KILIMANJARO
|
DKT. BEST MAGOMA
|
0754-621046
|
|
8.
|
LINDI
|
DKT. SONDA YUSUPH
|
0653-384350
|
sonda_y@yahoo.com
|
9.
|
MANYARA
|
DKT. SUNGWA KABISSI NDAGABWENE
|
0713-450765
|
Mas19730ok@yahoo.co.uk
|
10.
|
MARA
|
DKT. SAMSON WINANI
|
0784-450425
|
sam.winani@yahoo.co.uk
|
11.
|
MBEYA
|
DKT. SEIF MHINA
|
0767-832275
|
sbmhina@gmail.com
|
12.
|
MOROGORO
|
DKT. JACOB FRANK
|
0767-985850
|
|
13.
|
MTWARA
|
DKT. WEDSON SICHALWE
|
0755-048787
|
|
14.
|
MWANZA
|
DKT. LEONARD SUBI
|
0784-501020
|
subileon@yahoo.com
|
15.
|
PWANI
|
DKT. BEATRICE BYARUGABA
|
0784-319764
|
bykami@yahoo.com
|
16.
|
RUKWA
|
DKT. JOHN GURISHA
|
0784-216008
|
igurisha@yahoo.com
|
17.
|
RUVUMA
|
DKT. DAMAS KAYERA
|
0713-537495
|
dajkay@gmail.com
|
18.
|
SHINYANGA
|
DKT. NTULI KAPOLOGWE
|
0654-586346
|
nkapologwe2002@gmail.com
|
19.
|
SIMIYU
|
DKT. MAGEDA KIHULYA
|
0754-507875
|
mkihulya@yahoo.com
|
20.
|
SINGIDA
|
DKT. JOHN MWOMBEKI
|
0786-103225
|
johnmwombeki@yahoo.co.uk
|
21.
|
TABORA
|
DKT. GUNINI KAMBA
|
0783-344079
|
gunini@yahoo.com
|
22.
|
TANGA
|
DKT. ASHA MAHITA
|
0715-465521
|
ashamahita@yahoo.co.uk
|
23.
|
GEITA
|
DKT. JOSEPH KISALA
|
0788-046787
|
joskisala@gmail.com
|
24.
|
KATAVI
|
DKT. YAHYA HUSSEIN
|
0754-372772
|
hyahaya70yahoo.com
|
25.
|
NJOMBE
|
DKT. SAMUEL MGEMA
|
0757-226806
|
mgemasamuel@gmail.com
|
IMETOLEWA TAREHE 22/08/2016
No comments: